UNIVERSITY EXAMINATION (UE) WEEK

UNIVERSITY EXAMINATION (UE) WEEK

Aloooooh, Kimeumana! Nikisema kimeumana na maanisha mtu wangu wa nguvu bwana, leo kwenye ile segment yetu pendwa ya Uni Corner ni kama kwa motoo hivi, wanachuo wenyewe wanakwambia ni majonzi juu ya majonzi.

Hichi ndo kile kipindi ambacho ule msemo uliotumiwa sana na wahenga kuwa utavuna ulichokipanda ndo hiki sasa, ambapo kila mwanachuo anakumbuka kuwa familia inamtegemea, wenyewe wanakwambia ndio nyakati ya kujua malecturer wote ili uweze kutimiza coursework. 

Bwana vibe la leo kama limepoa flani hivi ila ndo hivyo kama ulikuwa hujui mtu wangu wa nguvu ni kwamba takribami vyuo vyote Dar es salam na nje ya jiji vikiwemo UDOM, UDSM, IFM nk, ambapo week hii wako katika mitihani ya kumaliza semester (muhula wa masomo)

Wanangu wa Mwananchi Scoop kama una ndugu yako yuko chuo na hajakwambia basi sisi tumekufikishia taarifa hii hadi kiganjani kwako, all in all, best wishes kwao.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags