Unicomedy show warudi na balaa zito

Unicomedy show warudi na balaa zito

Wanachuo mambo vipi? Holiday dizaini imekuwa ndefu, wengine tukiwa tumechill mtaani bila ishu yoyote na wengine wako kasi kukimbizana na  mambo ya field report basi ni trab na trat katika vichwa vya wanachuo aisee!

Basi ule wakati wa furaha kwa wanachuo ni pale tu bodi ya mkopo inapotia mkwanja kwa wanufaika wa boom vyuoni inakuwa shangwe yaani sio shida zetu kabisa, si unajua tena ukizipata pesa lazima kutumia au sio wasomi wenzangu? Ndio! Basi wanachuo wote kwenye vyuo tofauti tofauti hukutana sehemu moja tu kwa ajili ya kufurahi na kushusha mzigo wa stress ndani ya show la kibabe Unicomedy.

Unicomedy show ni platform inayohusika na sanaa ya uchekeshaji maarufu “Stand-up comedy”show hii hutembelea vyuo mbalimbali ndani ya Dar es salaam kila mwisho wa week, vilevile hufanyika show kubwa inayowakutanisha wanachuo wote na wapenzi wa comedy na kwa wale ambao washawahi kufika kwenye show zao wanajua balaa lao.

Aloooooh! This time Unicomedy show wanarudi na moto baada ya kukaa kimya  kwa takribani miezi 10 bila kufanya show vyuoni. Kupitia ukurasa wa Instagram wa unicommedy wametoa taarifa kwamba tarehe 1st  October, 2022 wana jambo lao na watazungumza na waandishi wa habari.

Je unafikiri jambo lenyewe ni lipi? Tuliaa hapa kwenye UniCorner ndani ya Mwananchi Scoop kwa taarifa zaidi.

Until next time byee!!

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Habiba Mohamed

A digital journalist and writer for mwananchi scoop My stories around entertainment,fashion, Artist profile, relationship, lifestyle and career.


Latest Post

Latest Tags