Undani wa matatizo ya akili baada ya kujifungua (Post - Partum)

Undani wa matatizo ya akili baada ya kujifungua (Post - Partum)

Msomaji wa saikolojia inayokujia kila siku ya Alhamis kupitia jarida la MwananchiScoop, leo nimekuja na mada kabambe inayohusu matatizo ya afya ya akili yanayotokea baada ya kujifungua (Postartum Psychosis).

Nafahamu kuwa wapo baadhi ya wanafunzi hupata mimba wakiwa chuoni na pindi wanapokumbana na changamoto mbalimbali husababisha kupata matatizo ya afya ya akili.

Hivyo basi kaa nami leo kujua ugonjwa huu ni nini na unatokana na sababu gani hasa na ni watu wa aina gani huathirika zaidi na janga hili.

Matatizo ya afya ya akili baada ya kujifunga ni ugonjwa wa afya ya akili ambao wamama au msichana ana upata mara baada ya kujifungua mtoto.

Ni ugonjwa ambao huanza ghafla baada ya kujifungua, unatokea ndani ya siku au wiki baada ya kupata mtoto. Watu wengi ambao wamejifungua hupata mabadiliko ya mhemko baada ya kupata mtoto anayejulikana kama "mtoto blue," hii ni kawaida na hudumu kwa siku chache.

DALILI ZA KISAIKOLOJIA ZA UGONJWA HUO

Dalili ya kwanza huanza ghafla ndani ya wiki 2 za kwanza baada ya kujifungua ambayo ni kusikia, kuona, kunusa au kuhisi vitu ambayo havipo kabisa.

Nyingine ni ‘Amanic mood’ yaani mhemko huu hapa, mtu anaweza kuzungumza na kufikiria sana au haraka sana na kuhisi yuko juu ya hii dunia.

Dalili zingine ni kukosa nguvu, kukosa hamu ya kula, kuwa na wasiwasi muda wote, kupata shida wakati wa kulala au kuto kulala kabisa, kuhisi kuchanganyikiwa, kuhisi tuhuma pia kuwa na mawazo ya kujiuwa au kuuwa.

WATU AMBAO WAKO HATARINI KUPATA HUU UGONJWA

Mtu ambaye kwenye familia wana shida ya afya akili inakuwa rahisi kupata ugonjwa huu.

Mwingine ni yule wenye mabadiliko makubwa ya homoni maana huchangia sana kupata hii shida.

Lakini pia kutokutumia dawa za afya akili kama uliuugua au uliacha dawa pia upo hatarini kupata tena ugonjwa huu. 

USIMAMIZI WAKE KISAIKOLOJIA

Kwa sababu ya hatari kubwa ya kujiuwa au kuuwa mtoto mchanga, usimamizi wa saikolojia ya afya ya akili inahitajika kuendelea mara nyingi kwa wiki, mwezi.

Matibabu na dawa ni muhimu kutolewa kwa wakati ambao mgonjwa yupo katika usimamizi wa afya akili. Na hapa tunasisitiza kuwepo kwa mazingira salama kwa mama au binti na mtoto.

Pia mama apewe ushauri wa kukabiliana na hali aliyokuwa nayo na umuhimu wa kutumia dawa ili kupona kabisa tatizo hilo.

Matibabu ya kisaikolojia kama tiba ya kitabia ya utambuzi (CBT) au kisaikolojia ya kibinafsi (IPT) inter person therapy, inaweza kusaidia wanawake kukuza mikakati bora ya kukubaliana na tatizo hilo na kupona kabisa.

Tiba mama au binti na mtoto inaweza kuwa na faida katika kukuza kushimamia matibabu yaliyo bora kwa mama. Ushauri pia kwa familia inayomzunguka ni muhimu sana.

USHAURI

Tunapoona mtu amepata shida kama hii na kusambaa katika mitandao yote, tujitahidi kufiikiria nje ya box kuliko kulaumu.

Watu wenye shida hii sio kosa lao, wanapata shida ya afya ya akili kama nilivyoeleza hapo juu so wanahitaji support ya kimatibabu, upendo na kuthaminiwa.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags