Unaujua ubinafsi usio wa kawaida

Unaujua ubinafsi usio wa kawaida

Kila mtu ana tabia tofauti za ubinafsi. Tabia hizo ndizo ambazo mtu anavyofikira na kutenda kawaida, zinazomtofautisha yeye na  wengine.

Tabia za mtu hugeuka na kuwa ubinafsi usio wa kawaida wakati fikra au mienendo yake huwa imezidi kupita kiasi cha kawaida, kupindukia mpaka kuwa ngumu na isiyofaa.

Hii husababisha matatizo makubwa kwa maisha yake na kawaida inaunganisha na dhiki sana kwa yeye au wengine.

Ubinafsi usio wa kawaida huanzia utotoni na unaendelea hadi mtu anapobalehe. Haijulikani ubinafsi usio wa kawaida umeenea kwa kiasi gani. Kila aina ya ubinafsi wa ugeugeu umeenea kwa kiasi tofauti.

Ubinafsi wa ugeugeu huathiri mtu mmoja kati ya watu mia moja. Ingawaje tabia au ubinafsi wa mtu sio rahisi kubadilisha.

Zipo aina mbalimbali za ubinafsi usio wa kawaida ambazo ni

Ubinafsi wa kutokwamini wengine

Hili ni kundi la magonjwa ya haiba ambapo mtu hutawaliwa na hali endelevu ya kuhisi kuongelewa na watu au kutoamini wengine.

Kundi hili la watu hawapo tayari kusimamia jukumu la hisia zao na kupenda kuona wengine ndo wanahusika na jukumu hilo. Watu wa kundi hili huweza kuwa wakali na kutawaliwa na wivu mkali "pathological jealous".

Watu hawa hujawa na hisia za kuona wakisalitiwa au kutowaamini kabisa wapenzi au wenza wao. Hivyo mara nyingi hukumbana na migogoro katika mahusiano wanayoyaanzisha.

Ubinafsi wakujitenga

Hii ni hali ambayo aliyeathiriwa hujitenga na jamii na huwa anaonyesha hisia mbalimbali chache sana kwa watu wengine.

Ubinafsi wa kujitenga pia ni hali ambayo mtu anakuwa na ukosefu wa uhusiano mzuri wa kijamii  na watu wengine mara nyingi pia  huwa na upotovu, uono na tabia zisizo za kawaida.

 

Ubinafsi wa kupenda

Ni hali ambayo mtu hutamani sana kutunzwa na wengine na kumfanya kuwa mtiifu kwa hofu ya kuwa atatengwa na kujiweka chini.

Pia ubinafsi huu umfanya mtu kuwa na tabia ya kujihatarisha, bila taratibu, kutokuwa na uhusiano mzuri na watu wengine pia hufikiri ubinafsi wake hauna umuhimu wowote.

Jamani mtu huyu huogopa kutengwa na kuachwa na wengine, huwa na fikira za vipindi vya hali ya kutowaamini wengine (paranoia) na hufikiri mambo yasiyo na uhusiano wowote na ukweli.

Ukumbuke kwamba binadamu anapoingiliwa na ubinafsi, basi maisha yake yameharibika   hata mambo yake yale mazuri aliyokabidhiwa na Mungu utoweka.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags