Umuhimu wa logo katika biashara yako

Umuhimu wa logo katika biashara yako

Wajasiliamali na wafanyabiashara wote nawasalimu kwa jina la Jamuhuri la Muungano wa Tanazania.., ni matumini yangu biashara zinaenda kama kawaida na kila kitu kiko pouwa.

Sichoki kuongea na nyie ndugu zangu maana najua kabisa hichi mnachokifanya ni kwaajili ya kufanikisha na kujikimu mahitaji yote, sasa bwana katika biashara leo tunazungumzia na kuelimishana kuhusu umuhimu wa logo katika biashara yako.

Logo ni alama au nembo iliyodizainiwa mahsusi kwa ajili ya biashara yako na inatumika kukutambulisha nje na ndani ya ofisi kwa maana nyingine tunaweza kusema  Logo ni alama au nembo inayotumika kutambulisha huduma, bidhaa, kampuni au mfumo wowote wa vikundi.

Logo au nembo inamaanisha vitu vingi kuhusu biashara yako kulingana na muonekano wake , biashara nyingi sana utambulisho wake hupatikana kwanza kwenye logo, matangazo  mengi hulenga watu kukumbuka lengo na logo ya biashara.

Logo ndio kitu ambacho mtu hufikiria anaposikia jina la kampuni au biashara yako.

Mfano, Unaposikia jina Cocacola, Azam, TBS, Vodacom, Pepsi, Asas nk. Kitu cha kwanza kitakachokuja kwenye kichwa chako ni logo ya kampuni kisha matangazo uliyokwisha yasikia au kuyaona kuhusiana na huduma au bidhaa zao huanza kujirudia kichwani pindi tu utakapo yaona. Hivyo basi logo ni  muhimu sana kwa maendeleo au mafanikio ya biashara yako.

  • Humpa mteja maana au tafsiri ya biashara yako
  • Huonyesha muonekano unaotakiwa
  • hukuongezea hadhi ya biashara
  • Huonyesha utofauti wako na wengine katika soko
  • Kuwa na muonekano wa kuvutia
  • Logo husaidi mteja kutamani kununua bidhaa hata kama hajaiona, mfano Azam ukiona tangazo na logo yake lazima utatamani tu kupata bidhaa yake.
  • Husaidia biashara yako kujulikana nchi nzima na katika mitandao yote ya kijamii 

Sababu kwanini biashara yako inahitaji logo, kuna sababu nyingi kwanini biashara yako iwe na logo tena sio logo tu iwe na logo iliyodizainiwa vizuri, baadhi ya sababu za msingi ni pamoja na

Kutengeneza Logo nzuri sio kufanya biashara sijui tumeelewana hapa nikiwa na maana kuwa, bidhaa yako ikiwa bora basi Logo na nembo yako itajitembeza yenyewe mitandaoni na sehemu mbalimbali kwasababu ubora na uzuri wako katika biashara ndo kufanya jina la biasharea yako kujulikana. 

Mifano yote ya Logo tulioitaja hapo juu imejulikana kwasababu ya ubora na uzuri wa bidhaa zake so jitahidi katika biashara ziwe na ubora ili uweze kupata wateja wengi kupitia hao hao wateja wako, bidhaa ikipendwa na mteja mmoja basi yeye ndo atakuwa kama ambassador wako niamini  kwa hili.

 


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post