Umuhimu wa Lipstick kwenye midomo yako

Umuhimu wa Lipstick kwenye midomo yako

Naam!! kama kawaida yetu tunakaribishana tena katika ulimwengu wa Fashion ili uweze kujua  urembo na mitindo mbalimbali inayobamba kwa sasa katika fashion.

Leo katika fashioni nikusihi sana usijaribu kukwepa, maana tutagusia namna nzuri ya kupaka Lipstick ili uweze kutunza ‘lipsi’ zako na kuzifanya ziwe na muonekano wa kisasa wenye kuvutia unaoenda na wakati.

Kama tunavyofahamu wanawake wengi warembo na wanaojiamini katika fashion lazima wahakikishe wanakuwa na muonekano mzuri kuanzia mavazi na lips zao, lakini jambo ambalo unatakiwa kujua ni kwamba ukipaka lipstick inasaidia kutunza lipsi zako wakati wote.

Lazima utambue kuwa midomo  ni sehemu muhimu sana katika kukamilisha unadhifu wako katika urembo na afya.

Fahamu kwamba ngozi ya midomo ni laini sana na inahitaji uangalizi wa hali ya juu, hakikisha inakuwa laini siku zote, kuna wale wapenzi wa kupaka mafuta kwenye lips zao kama mafuta ya mgando, vaseline, lipstick, lipshine, na wengine si watumiaji kabisa wa product zozote yaani huacha ngozi ya midomo kuwa mikavu na kusababisha vidonda.

Ngozi ya midomo inahitaji ‘Exfoliated’ yaani kutolewa ngozi ngumu ya juu, wengine kutoa ngozi hiyo hutumia mswaki na kisha kupaka Vaseline.

Ni vizuri zoezi hili likafanyika usiku wakati wa kulala, itakufanya ukiamka uwe na lips laini zenye kuvutia . kunywa maji mengi ya kutosha hii nayo pia husaidia lips kutokuwa kavu mara kwa mara na kuwa nyororo.

Pia matumizi ya lipstick kila wakati ni muhimu sana ila unatakiwa uwe na tahadhari katika kupaka lipstic hakikisha hautumii lipstick ambayo imepita muda wa matumizi eti kwa sababu ya urembo kumbe unahatarisha lips zako kuharibika na kuwa na vindonda.

Zingatia upakaji wa lipstiki kwenye lipsi zako

 

*Hakikisha unatumia brush safi na salama ya lipstick kupaka kwenye midomo yako hii itasaidia kutumia kiasi kidogo cha lipstick maana ikiwa nyingi sana inapoteza muonekana mzuri kwenye lips zako.

*Ikutanishe midomo yako kabla ya kupaka,  hii itasaidia idumu kwa muda mrefu kwenye midomo yako bila ya kutoka kwa haraka.

*Paka kwa mbali ‘lipgloss’ lipshine ili kung’arisha midomo yako ila siyo lazima, kama haupendi unaweza kuiacha lipstick tu yenyewe.

Namna nzuri ya kupaka kwenye midomo yako/ lips

-Anza kwa kupaka kilainishi kabla ya kupa lipstick (Lipbam)

-Paka ‘lip liner’ ya colour ya lipstick ambayo unatarajia kupaka, hapa watu wa fashion nadhani mmenielewa sana.

-Chukua lipstick yako ukianzia kupaka lips za chini ukifuatwa za juu ili kuichanganya ya chini kama kawaida.

-Kuna wale wanaopenda kupaka double colour kwa ajili ya kupata muonekano wa kisasa siyo mbaya ukapangilia rangi zako ili uweze kupata muonekano bomba.

Baadaya kufuata hatua hizo utakuwa umekamilisha upakaji mzuri wa lipstick katika midomo yako na kuifanya ya kuvutia na yenye Afya.

 

Angalizo, angalia katika upakaji wa lipstick kuchagua rangi ambayo inashabihiana na ngozi yako ili usije ukaonekana kituko.

Pia hii ni muhimu kujua ubora wa lipstick yako kabla haujapaka na muda gani inatakiwa itumike yaani angalizo la lipstick kuisha matumizi yake isije ikakuharibu midomo yako badala ya urembo ukaharibika.

Kwa leo acha nikwamie hapo ili nikupe muda wa kwenda kuyafanyia kazi haya ya leo tukutane tena hapa kwenye magazine ya Mwananchi Scoop next week.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags