Umuhimu wa kuchukua likizo kazini

Umuhimu wa kuchukua likizo kazini

Na Aisha Lungato

Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya Mwaka 2008 kifungu namba 31 ibara (1) imeeleza kuwa Mwajiri atatakiwa kutoa likizo kwa mfanyakazi angalau siku 28 mfululizo kuhusiana na kila mzunguko wa likizo, na likizo hiyo itajumuisha siku yoyote ya sikukuu ambayo inaweza kuangukia ndani ya kipindi cha likizo.

Ukiachilia mbali na sheria hiyo pia, Sheria ya Ajira na Mahusino kazini (Employment and Labour Relation ACT No. 6 ya mwaka 2004 imesisitiza kuwa “mfanyakazi ana haki ya kukataa au kutofanya kazi wakati yupo likizo ya mwaka”

Lakini hili limekuwa likikaidiwa na baadhi ya wafanyakazi kutotaka kabisa kwenda likizo kutokana na kuhofia nafasi zao kuchukuliwa na watu wengine.

Hivyo basi kwa mapitio haya ya sheria mbalimbali zinatukumbusha kuwa kila mfanyakazi katika kampuni au taasisi yoyote anayohaki ya kupata likizo kwa wakati sahihi. Na huu ndiyo umuhimu wa likizo mahala pa kazi.

  1. Kupanua fikra pamoja na mtazamo wako

Kitu ambacho watu wengi wameshindwa kukigundua ni kuwa kuchukua likizo kunaweza kukusaidia kupanua fikra zako na kuingiza mtazamo chanya, kuendelea kubaki katika mazingira zoefu kunaweza kusababisha akili yako kuganda yaani kunauwezekano akili yako ikashindwa kufikiri vitu vingine zaidi ya hivyo.

Kuchukua likizo na kwenda sehemu ya mbali either mkoa, au nchi nyingine kutakusaidia kutafakari vitu mbalimbali katika maisha yako ya kazini na kibinafsi na kuona nini cha kubadilisha na nini cha kubakisha.

  1. Kupunguza Msongo wa Mawazo

Siku zote tunajua kazi zimejawa na strees ambazo zinakusababishia msongo wa mawazo yasiyofutika akilini mwako ambapo tatizo hilo linaweza kukusababishia magonjwa kama ugonjwa wa moyo, kupata tatizo la afya ya akili pamoja na kuwa na asilimia kubwa ya kupata ajali uwapo barabarani.

Hii yote inasababishwa na kutopumzika kwa muda mrefu hivyo basi kuchukua likizo mara kwa mara kunaweza kukusaidia kwa asilimia kubwa kujiepusha na matatizo kama hayo.

  1. Kunakuongezea ufanisi kazini/ utendaji bora wa kazi

Kwa mujibu wa Utafiti uliofanyiwa na ‘Florida State University’ miaka saba iliyopita unaeleza kuwa wafanyakazi wanaoenda likizo zaidi ndiyo watu wana nafasi kubwa zaidi ya kupandishwa cheo pamoja na kufanikiwa kuliko watu wasiokwenda likizo.

Utafiti huu unathibitisha kuwa upatapo wakati kwa kupumziki kwa kwenda sehemu mbalimbali kunaweza kukufanya ukapata mawazo ambayo yanauwezo mkubwa kwa kuisaidia kampuni pindi utakapo rudi kazini.

  1. Kuongeza ubunifu

Kitu ambacho nimekigundua, mfanyakazi anapotoka likizo na kurudi kazini anakuwa na mawazo mathubuti ambayo yanauwezo wa kuitoa kampuni katika sehemu moja na kuipeleka sehemu ya juu zaidi huku utendaji wake wa kazi unakua si ule alioondoka nao, hii inakuja baada ya kupata wasaa wa kupumzika na kuzunguka sehemu tofauti tofauti.

Ukweli ni kwamba kupumzika kunaupa ubongo wako wakati wa kufikiri vitu vyenye manufaa zaidi.

Si hayo tuu pia kupata likizo ya mapumziko kunamsaidia mfanyakazi kuwa na furaha kutokana na kukutana na vitu tofauti tofauti, cha kuzingatia ni siyo lazima likizo yako iwe ya gharama kubwa hata kutumia wakati wako nyumbani kusoma vitabu, kuangali movie pamoja na documentary mbalimbali pia kunaweza kusaidia kuongeza kitu akili mwako.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post