Ukikubali kuoa/kuolewa unalipwa zaidi ya Sh 102 Milioni

Ukikubali kuoa/kuolewa unalipwa zaidi ya Sh 102 Milioni

Ukiwa ni muendelezo wa kukabiliana na kiwango cha chini cha uzazi nchini Korea Kusini, Wilaya ya Saha, Busan inampango wa kuwalipa wakazi wa eneo hilo watakao kubali kuchumbiana na kuoana.

Kwa mujibu wa tovuti mbalimbali nchini humo zimeeleza kuwa wilaya hiyo itawalipa wakazi dola 38,000 ikiwa ni zaidi ya Sh 102 milioni kwa wapenzi watakao kubali kufunga ndoa na kupata watoto.

Mpango huu ni sehemu ya mkakati mpana wa kukabiliana na kupungua kwa idadi ya watu nchini, hali ambayo imefikia kiwango cha hatari huku kiwango cha uzazi kikishuka hadi watoto 0.72 kwa kila mwanamke.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post