Ujio wa Idris Elba wafanya Anko Zumo awatulize waigizaji

Ujio wa Idris Elba wafanya Anko Zumo awatulize waigizaji

Baada ya mwigizaji kutoka Uingereza, Idris Elba kutangaza kuhamia Afrika katika kipindi cha miaka 10 ijayo kwa lengo kukuza tasnia ya filamu huku akitaja maeneo atayoishi ikiwemo Visiwani Zanzibar, Accra nchini Ghana au Freetown huko Sierra Leone, mwigizaji nchini Mohamedi Omari ‘Anko Zumo’ amewataka wasanii wa Bongo kuacha ujuaji pindi Elba atapotia timu nchini .

“Kwanza kabisa ni kheri nampokea kwa mikono miwili, nikiwa kama mwigizaji naona kikubwa atatusaidia kutupa vitu vipya ambavyo hatuvifahamu, lakini vilevile kututangaza kwa sababu yeye ni mkubwa na anatambulika na dunia nzima.

“Kwa upande wetu atatusaidia kufikisha hichi tulicho nacho na kile ambacho yeye atatuongezea kufika mbali na kujulikana zaidi. Ushauri wangu tumpe ushirikianao, tusilete ujuaji tumsikilize hata kama tunajua tujifanye hatujui ili tujue zaidi,tujifanye hatujui hata kama tunajua,”amesema Anko Zumo

Hata hivyo aliweka wazi kuwa anatamani Elba akitua nchini aanze katika upande wa soko na mauzo ya filamu

“Tunaonekana tunatengeneza filamu za hovyo hii ni kulingana na mauzo inamaana manunuzi yetu sisi hayatufanyi tutanue mabawa zaidi tukitaka kutengeneza filamu za Ulaya inabidi kutumia mandhari ya Ulaya mambo kama hayo sisi kwetu inakuwa ngumu sana labda yeye ashauri tasnia nzima kama ni bodi ya filamu, Wizara ya Sanaa nzima.

“Wasanii sisi tupo wengi sana lakini kilio chetu kazi zetu haziuziki, na utakuta anayenunua ndio anayesambaza sasa je tutaposema wasanii mauzo madogo unafikiri ataipeleka hiyo mjini hatoipeleka,”amesema

Utakumbuka kuwa Idris Elba alizaliwa London nchini Uingereza amewahi kuonekana katika filamu kama Beast, Extraction 1&2, Concrete Cowboy, Fast & Furious Presents: Hobbs & Shaw, Three Thousand Years of Longing, A Hundred Streets.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags