Ujauzito wa Britney Spears waharibika

Ujauzito wa Britney Spears waharibika

Pop Staa Britney Spears (40) na mpenzi wake Sam Asghari (28) amethibitisha kuharibika kwa mimba yake hivyo kumpoteza mtoto wao waliomtarajia.

Kupitia Instagram yake, Britney amethibitisha hilo kwa kuandika kuwa ana huzuni kubwa na analazimika kutangaza kwamba amempoteza mtoto wake.

“Kwa huzuni mkubwa tunalazimika kutangaza kwamba tumempoteza mtoto wetu mapema katika ujauzito, huu ni wakati wa huzuni kwa mzazi yeyote, labda tulitangaza mapema sana kuwa tunategemea kupata mtoto.

“Hata hivyo tulifurahi sana kuwapa habari njema muda huo, upendo wetu kwa kila mmoja ndio nguvu yetu, tutaendelea kujaribu kupanua familia yetu nzuri,” aliandika






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags