Ugonjwa wa Celine Dion ulimuanza mwaka 2008

Ugonjwa wa Celine Dion ulimuanza mwaka 2008

Mwanamuziki wa Canada Celine Dion, ameweka wazi kuwa ugonjwa aliokuwa nao wa ‘Stiff Person Syndrome’ ulianza kumsumbua toka mwaka 2008.

Dion ameyasema hayo wakati akiwa kwenye mahojiano na Hoda Kotb katika kipindi cha ‘Today Show this week’ ambapo amefichua kuwa alianza kupata dalili za ugonjwa huo miaka 17 iliyopita kabla hajatangaza kwa umma.

Aidha alieleza kuwa aliamua kutangaza tatizo hilo kutokana na kuelemewa na mizigo kama vile kulea watoto wake alioachiwa na marehemu mumewe René Angélil aliyefariki kwa saratani mwaka 2016, hivyo basi alitamani kuwashirikisha watu waweze kujua hali anayoipitia.

Mkali huyo wa ngoma ya ‘My Heart Will Go On’ mwenye umri wa miaka 56 alitangaza kusumbuliwa na ugonjwa huo Desemba 2022, na kumfanya aghairishe ziara zake.

Mbali na hayo siku kadhaa zilizopita Celine Dion aliweka wazi ujio wa filamu yake iitwayo ‘I Am: Celine Dion’ inayotarajiwa kuachiwa Juni 25 mwaka huu kupitia Amazon Prime Video, filamu hiyo itaonesha vita yake na ugonjwa huo ambao haujulikani kwa umma.

Ukiachilia mbali msanii huyo kuja na filamu hiyo, Mei 30 mwaka huu chanzo cha karibu cha msanii huyo kiliripoti kuwa Celine atatumbuiza kwa mara ya mwisho katika kipindi maalumu cha Tv huku ikielezwa kuwa kwa sasa amekuwa akifanya kazi na wakufunzi wa sauti, watu wa bendi na wataalamu kwa zaidi ya miezi sita sasa ili kulikamilisha hilo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags