Ugomvi wa wanandoa wasababisha ndege kutua kwa dharura

Ugomvi wa wanandoa wasababisha ndege kutua kwa dharura

Ndege ambayo ilikuwa njiani kutoka Munich, Ujerumani kuelekea Bangkok, ambao ni Mji Mkuu wa Thailand, imelazimika kutua kwa dharura katika Uwanja wa Ndege wa Indira Gandhi nchini India, kufuatia ugomvi ulioibuka baina ya wanandoa.

Kwa mujibu wa maofisa wa usafiri wa anga katika kiwanja hicho, ndege hiyo ilitua siku ya Jumatano kutokana na mgogoro kati ya mume na mke.

Shirika la ndege la Lufthansa, limesema katika taarifa yake jana kuwa wanandoa hao waliondolewa ndani ya ndege hiyo baada ya kutua India, hivyo kulazimika kukatiza safari yake ya Bangkok na kwamba "aliomba msamaha.''

Inasemekana baada ya vurugu hizo ambazo zinadaiwa kutishia usalama wa abiria na wafanyakazi, marubani wa ndege hiyo, awali waliomba ruhusa ya kutua Pakistan, lakini baada ya kushindikana, waliirusha hadi Delhi na kumkabidhi mwanaume huyo kwa maofisa wa usalama wa Delhi, India.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags