Ufilipino, IGP ajiuzulu baada ya askari wake kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya

Ufilipino, IGP ajiuzulu baada ya askari wake kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya

Mkuu wa Jeshi la Polisi, Jenerali Rodolfo Azurinjr amesema anachukua uamuzi wa Kuwajibika kama Kiongozi ili kuwahimiza Maafisa wengine 1000 kujiuzulu ili kurejesha Imani ya Umma kwa Polisi

Waziri wa Mambo ya Ndani,  Benjamin Abalos, alitoa wito kwa Majenerali wote wa Polisi na Makanali kujiuzulu kwa hiari ikiwa ni hatua kali ya kuboresha taswira ya Jeshi la Polisi kutokana na Maafisa wake kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya  

Jeshi la Polisi limekuwa likilaumiwa kukosa Nidhamu licha ya kuundwa Tume za Uchunguzi dhidi yake na kuwafungulia mashtaka Maafisa wanaotuhumiwa kwa Mauaji holela ya Wahalifu na Washukiwa wa Dawa za Kulevya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags