Ufahamu mti unaotiririsha maji

Ufahamu mti unaotiririsha maji

Waswahili husema kuishi kwingi, kuona mengi, pasi na shaka kauli hii inaendana na maajabu ya mti unaotiririsha maji.

Wengi wamezoea kuona miti ikipandwa, ikikua, ikikauka na mwisho kukatwa au kukatika yenyewe na mingine kukauka, lakini hii ni tofauti kwa mti unaotirirsha maji kama bomba.

Mti huo ni wa Mkuyu unapatikana katika kijiji cha Dinoša, Montenegro Kusini-Mashariki mwa Ulaya, huwa na kawaida ya kutiririsha maji ardhini yakitoka chini ya mizizi.

Tukio la mti huo kutiririsha maji kwa mara ya kwanza lilionekana mwaka 1990. Aidha kwa mujibu wa tovuti ya News 18 tukio hilo la mti kutiririsha maji ardhini huonekana mara moja kwa mwaka hasa katika kipindi cha mvua nyingi (masika).

Mti huo wa mkuyu unakadiriwa kuwa na miaka 100 hadi 150, huku ikidaiwa kuwa huenda katika mti huo kuna chemchem chini ya mizizi inayopelekea maji kupanda juu na kutiririka kupitia sehemu yenye uwazi.
.
.
.
#MwanannchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags