Ufahamu mtaa ambao kila mkazi anamiliki Ndege

Ufahamu mtaa ambao kila mkazi anamiliki Ndege

 Katika mitaa tunayoishi tumezoea kuona wakazi wa eneo husika wakimiliki vifaa vya usafiri mbalimbali vikiwemo Gari, Baiskeli pamoja na pikipiki lakini ni nadra sana kuona mtaa ambao kila mkazi anamiliki Ndege.


Lakini imekuwa tofauti katika eneo
la Cameron Park, California, nchini Marekani ambapo asilimia kubwa ya wakazi katika eneo hilo wanamiliki ndege kuliko magari, huku maegesho ya ndege hizo yakiwa pembeni mwa nyumba zao.


Kitongoji hicho ambacho kinajulikana zaidi kama Cameron Airpark Estates, kilianzishwa rasmi mwaka 1963 ambapo mpaka kufikia sasa kinadaiwa kuwa na zaidi ya nyumba 120.


Wakazi wa eneo hilo wanauwezo wa kupaki ndege zao bila kutokea changamoto yoyote kutokana na barabara za mitaa hiyo kujengwa kwa upana mkubwa.


Licha ya eneo hilo kuwa la kuvutia zaidi pia linatajwa kuwa eneo lenye vivutio vingi ambapo wakazi wake wengi wanadaiwa kuwa Marubani huku majina ya barabara za mitaa hiyo yakiwa ni ya makampuni yanayojishughulisha na uundaji wa ndege ikiwemo Boeing Road.

.
.
#mwananchiscoop
#burudikanasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post