Tyson haogopi kuzichapa na Jake

Tyson haogopi kuzichapa na Jake

Bondia wa ngumi za kulipwa Mike Tyson ambaye anatarajia kuzichapa mwezi Julai mwaka huu na bondia chipukizi Jake Paul, amefunguka kuhusu hofu yake na jinsi anavyoweza kukabiliana nayo.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni na Sean Hannity, Tyson alieleza  kuwa haogopi pambano lake na Jake kwani huwa anachokiogopa ndicho anachikifanya, huku akiweka wazi kuwa aliwahi kuogopa pambano moja tuu la Roy ambalo alizichapa na Jones Jr mwaka 2020.

Aidha Mike aliendelea kwa kueleza kuwa kwa sasa anachokiogopa ni kifo tu na siyo pambano lake lolote, hivyo basi yupo tayari kuzichapa na Jake.

Tyson (57) anatarajia kuingia ulingoni na Jake Paul (27) katika uwanja wa AT&T uliopo jijini Texas pia pambano hilo litaonesha Mubashara (live) kupitia #Netflix.
.
.
.#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags