Tyson Fury atumia saa kutangaza pambano lake na Usyk

Tyson Fury atumia saa kutangaza pambano lake na Usyk

Bondia wa ngumi za kulipwa kutoka Uingereza, Tyson Luke Fury ametumia saa ya kifahari iliyotengenezwa na kampuni ya Jacob & Co kutangaza pambano lake na bondia kutoka Ukraine Oleksandr Usyk.

Pambano hilo la kugombea taji la uzito wa juu linatarajiwa kufanyika Mei 8 mwaka huu jijini Riyadh, Saudi Arabia, ambapo ndani ya Saa hiyo imeonesha masanamu mawili ya wapiganaji hao.

Mshindi katika pambano hilo atatambulika kama bingwa asiyepingwa wa uzani wa juu wa kwanza toka nafasi hiyo ichukuliwe na Lennox Lewis mwaka 1999.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post