Tyson Fury aliondoka na mkwanja wa maana pambano lake na Usyk

Tyson Fury aliondoka na mkwanja wa maana pambano lake na Usyk

Ingawa bondia wa ngumi za kulipwa Tyson Fury kashindwa pambano lake na Oleksandr Usyk lakini ameripotiwa kuwa alikuwa mshindi kifedha baada ya kuondoka na dola milioni 100 ikiwa ni sawa na Sh 259 bilioni huku mshindi Usyk akiondoka na dola milioni 45 sawa na Sh 117 bilioni.

Ikumbukwe kuwa wawili hao walizichapa Mei 18, 2024 katika uwanja wa Kingdom Arena mjini Riyadh, Saudi Arabia, ambapo mabondia hao walikuwa wakiisaka rekodi ya ‘Undisputed Champion’ iliyokuwa ikishikiliwa na #LennoxLewis tangu mwaka 1999.

Kupitia pambano hilo bondia kutoka Ukraine, Oleksandr Usyk aliibuka kidedea kwa kumchapa Fury na kufanikiwa kuondoka na mkanda huo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags