Tyla awajibu wanaomfananisha na Rihanna

Tyla awajibu wanaomfananisha na Rihanna

Japo siyo mbaya mtu kulinganishwa na mtu mwingine lakini kwa mwanamuziki kutoka nchini Afrika Kusini Tyla ameonekana kutopendezwa na suala hilo, hii ni baada ya wadau kuunganisha  picha yake na ya mwanamuziki kutoka katika visiwa vya Barbados, Rihanna na kusababisha awatolea uvivu kwa kudai hawezi kufanana.

Tyla ameyasema hayo katika jarida la Cosmopolitan ambapo alieleza kuwa hakatai kufananishwa na Riri lakini kwasasa anachokihitaji ni yeye kujulikana mwenyewe kupitia muziki wake na siyo vinginevyo.

“Watu wanataka kunishindanisha na mtu ambaye wanamjua lakini mimi napambana kufanya kitu ambacho hakuna mtu amewahi kufanya hapo awali na hakiwezi kulinganishwa na mtu yoyote” amesema Tyla

Hata hivyo kupitia jarida hilo alizungumza kuhusiana na baadhi ya mashairi yaliyopo kwenye wimbo wa ‘Water’ ambayo baba yake mzazi hakuyaelewa na kutokukubaliana na wimbo huo lakini baada ya kushinda tuzo ya Grammy 2024 ndipo akaelewa.

Mwanamuziki huyo mwenye umri wa mika 22 tayari ameachia albumu yake ya kwanza iliyopewa jina la ‘Tyla’ aliyoitoa Machi 22 Mwaka huu ambayo alimshirikisha Tems na Travis Scott, huku wimbo wake wa ‘Water’ ukishika namba saba kwenye Billboard Hot 100.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags