Trey aikwepa kesi ya unyanyasaji wa Kingono

Trey aikwepa kesi ya unyanyasaji wa Kingono

Imeripotiwa kuwa mwanamuziki kutoka nchini Marekani, #TreySongz amemalizana na kesi yake ya unyanyasaji wa kingono ambayo ilifunguliwa February mwaka 2016.

Kwa mujibu wa Daily Mail News, imeeleza kuwa mwanamke mmoja ambeye jina lake halikufahamika alijitokeza na kudai kuwa Trey alimfanyia vitendo hivyo kwenye kumbi moja ya starehe mjini Los Angeles nchini humo.

Hata hivyo bado haijafahamika kama msanii huyo amelipa kiasi cha dola 25 million ambazo mwanamke huyo alitaka alipwe kwa kumsababishia matatizo ya akili na kihisia baada ya tukio hilo au amekutwa na hatia.

Ikumbukwe kuwa mwaka jana Trey aliutumia ukurasa wake wa #Instagram kujisafisha kwa kuandika kuwa uongo kamwe hauwezi kuwa ukweli.

Msanii huyo amewahi kufanya nyimbo kama ‘I can't help but I Wait’, ‘Love Faces’, ‘Na na’, ‘Say Aah, ‘Hart attack’, ‘Slow Motion’, ‘Brain’ na nyingine nyingi.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags