Trela ya Moana 2 yaweka rekodi

Trela ya Moana 2 yaweka rekodi

Trela ya animation ‘Moana 2’ imeweka rekodi ya kutazamwa na zaidi ya watu milioni 178 katika saa 24 tangu kuachiwa kwake na kuifanya kuwa trela ya kihistoria ambayo haijawahi kutokea katika filamu za Disney.

Filamu hiyo iliyoandaliwa na Walt Disney Animation Studios na Pstrong imezipiku filamu nyingine ambazo zilipata watazamaji zaidi ikiwemo Inside Out 2 (milioni 157), Frozen 2 (milioni 116) na Incredibles 2 (milioni 116).

Moana 2, inawakutanisha tena nyota wa sauti Auli’i Cravalho na Dwayne Johnson, huku ikitarajiwa kuanza kuoneshwa rasmi katika kumbi za sinema Novemba 27 mwaka huu.

Ikumbukwe kuwa toleo la kwanza la Moana lilitoka mwaka 2016 na kuingiza dola milioni 687 duniani kote huku ikiwa ndiyo filamu iliyofuatiliwa zaidi mwaka 2016.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags