Travis Scott kayakanyaga tena

Travis Scott kayakanyaga tena

Rapa Travis Scott ameripotiwa kukamatwa na polisi jijini Paris, Ufaransa kwa madai ya kumpiga mlinzi wake (Bodyguard).

Kwa mujibu wa Dail Mail, Scott amekamatwa alfajiri ya leo Agosti 9, 2024 katika hoteli waliyokuwa wamefikia yeye na mlizi wake huku polisi wakiweka wazi kuwa wakati wa ugomvi mwanamuziki huyo alikuwa amelewa.

Travis Scott amekwenda nchini humo kwa ajili ya nusu fainali za michuano ya Olimpiki ya mpira wa kikapu iliyofanyika siku ya jana ambapo USA ilikuwa ikicheza na Serbia.

Kwa mwaka 2024 itakuwa ni mara ya pili kwa Travis kukamatwa na polisi kwani miezi miwili iliyopita alikamatwa na polisi jijini Miami kwa kufanya vurugu wakati akiwa amelewa.

Hata hivyo jana Mahakama ilimfutia mashitaka hayo yaliyokuwa yakimkabili ya kufanya vurugu wakati akiwa amelewa, huku mahakama ikimuamuru kufika mahakamani Septemba 10, 2024 kwa kosa la kukatiza kwenye makazi ya watu na gari yake bila ridhaa yao.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags