Travis Scott azuiliwa kufanya show Misri

Travis Scott azuiliwa kufanya show Misri

Chama cha wanamuziki Misri siku ya jana kilipiga marufuku tamasha la mwanamuziki kutoka Marekani Travis Scott lililopangwa kufanyika Julai 28 kwenye piramidi za Giza.

Kwa mujibu wa Africanews inaelezwa kuwa, tamasha hilo limefungwa kutokana na kuzuka kwa wasiwasi juu ya usalama na imani za utamaduni wa Scott unaweza kuharibu desturi yao.

Chama cha Muziki Misri kimetoa taarifa isemayo,

“Kutokana na utafiti na habari zilizopo kuhusu matamasha ya Travis Scott imeonesha kutoendana na thamani na desturi za jamii yetu. Kwahiyo Bodi ya Wakurugenzi imeamua kufuta kibali cha show iliyokuwa ifanyike Julai 28 kwenye Piramidi”.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags