Travis Scott aachiwa huru kwa dhamana

Travis Scott aachiwa huru kwa dhamana

Mwanamuziki Travis Scott ameripotiwa kuachiwa huru kwa dhamana, baada ya kukamatwa siku ya Jana Alhamis asubuhi kwa kosa la ulevi kupindukia.

Kwa mujibu wa tovuti ya Cnn, Travis alifanikiwa kuachiwa huru kutoka katika kituo cha polisi cha Guilford Knight baada ya kutoa dhamana ya dola 650 sawa na Sh 1.5 milioni.

Bradford Cohen ambaye ni mwanasheria wa Scott aliweka wazi sababu ya msanii huyo kuwekwa kizuizini kwa muda mfupi ni kutokana na kutoelewana na watu waliyokua eneo la tukio, lakini hakukuwa na shambulio lolote la majeraha ya kimwili.

Hii ni mara ya pili kwa Travis kukamatwa na polisi, mara ya kwanza alitiwa nguvuni wakati wa onesho lake la ‘Lollapalooza’ mwaka 2015 na kuhukumiwa mwaka mmoja.

Utakumbuka kuwa ndani ya wiki hii naye mwanamuziki wa Marekani Justin Timberlake aliripotiwa kukamatwa na polisi baada ya kukutwa anaendesha gari akiwa amelewa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags