TPLB yatupilia mbali rufaa ya mchezaji aliyempiga mwenziye kiwiko

TPLB yatupilia mbali rufaa ya mchezaji aliyempiga mwenziye kiwiko

Kamati ya usimamizi na uendeshaji wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPLB) imetupilia mbali rufaa ya ‘klabu’ ya #Yanga ya kutaka marejeo (review) ya adhabu ya mchezaji wao #KhalidAucho ambaye amefungiwa michezo 3 na faini ya Tsh laki tano.

Mchezaji huyo alifungiwa kwa kosa la kumpiga kiwiko kiungo wa ‘klabu’ ya #CoastalUnion, #IbrahimAjibu kwenye mchezo uliochezwa Novemba 08, 2023.

Baada ya kupitia shauri la Yanga na kanuni za Ligi, Kamati hiyo imejiridhisha kwa mara nyingine kuwa adhabu iliyotolewa kwa mchezaji huyo ni sahihi hivyo anapaswa kuendelea kuitumikia, huku ikimtaka mchezaji huyo kuzingatia mchezo wa kiungwana wakati wote.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags