Tory Lanez kutoa ushahidi Mahakamani

Tory Lanez kutoa ushahidi Mahakamani

Rapa Tory Lanez anatakiwa kufika mahakamani Desemba 14, mwaka huu kwa ajili ya kutoa ushuhuda wa tukio lake la kumshambulia kwa risasi mbili mguu mwanadada Theestallion.

Rapa huyo alifanya shambulizi hilo Julai mwaka jana na mashtaka anayoshtakiwa nayo uwenda yakamuweka miaka 22 gerezani.

Hata hivyo Tory Lanez anaripotiwa kukataa kuingia makubaliano na waendesha mashtaka kwenye kesi hiyo inayomkabili.

Wakili wa Rapa huyo Shawn Holley mapema jana alifika mahakamani na kukubali kwamba watafika tarehe hiyo iliyotajwa kwa ajili ya kusikiliza kesi hiyo ambapo Tory Lanez atatakiwa kutoa ushahidi wa takribani dakika 90.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags