Tory Lanez hayupo kwenye gereza la peke yake

Tory Lanez hayupo kwenye gereza la peke yake

Baada ya kuzuka kwa taarifa kuwa ‘Rapa’ kutoka nchini marekani Tory Lanez kuwa amefungwa katika ‘selo’ ya peke yake kutokana na umaarufu wake, taarifa za hivi karibuni zinaeleza kuwa msanii huyo kwa sasa hayupo tena kwenye ‘selo’ ya peke yake.

Kwa mujibu wa TMZ inaeleza kuwa wamepata taarifa kutoka gereza hilo likieleza kuwa msanii huyo anatumia asilimia 96 ya ratiba ya wafungwa wa kawaida na endapo mambo yataenda sawa atapata fursa ya kupata elimu inayotoa vyeti na ‘digrii’ za uzamili.

Hata hivyo timu ya wanasheria wake inasisitiza msanii huyo asichangamane na watu muda wa kutoka nje ambapo afisa mmoja alisema kuwa hakuna ulinzi wa ziada kwake kwani ni mfungwa wa kawaidia kama wengine.

Ikumbukwe Tory Lanez anatumikia kifungo cha miaka 10 kwa makosa matatu ambapo moja wapo likiwa ni kumpiga risasi aliyekuwa mpenzi wake Megan Thee Stallion.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags