Tory azungumza kwa mara ya kwanza tangu aingie gerezani

Tory azungumza kwa mara ya kwanza tangu aingie gerezani

Baada ya ku-trend kwenye mitandao ya kijamii kuhusiana na ‘rapa’ Tory Lanez ambaye kwa sasa yuko gerezani kuwa anahofia maisha yake, hatimaye ‘rapa’ huyo amezungumza na kueleza kuwa anafurahikia maisha yake na wala hana tatizo lolote.

Tory amewatoa hofu mashabiki wake baada ya ku-share sauti hiyo inayosikika akieleza kuhusiana na kuondolewa kwenye gerezani la North Kern State, Delano, California ambalo lilikuwa halimtendei haki kwa kumuweka ‘selo’ ambayo haina madirisha wala vioo.

Licha ya hayo ameahidi mashabiki wake waliokuwa wakisubiri kazi zake, kuwa sasa ziko tayari na watarajie siku si nyingi zitaanza kuachiwa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags