Tips za kupangilia muonekano wako

Tips za kupangilia muonekano wako

Hellooow! Guyz kama tulivyo waambia hapo mwanzo kuwa mwananchiscoop itakuwa inaruka kila siku ya ijumaa ikiwa imesheheni mambo kedekede na leo bwana kwenye dondoo za fashoon, Nimekuletea mambo ambayo yatakufanya kuwa na mwonekano bomba kabisa. 

  1. VAA NGUO ZINAZO ENDANA NA UMBO NA KUKUTOSHA

tafuta nguo zinazo kutosha na kuendana na mwili wako kuvaa nguo ambayo inakaribia kukutosha au haikutoshi kabisa haileti muonekano mzuri pia kuvaa nguo inayo bana sana tofauti na umbo lako. Vaa kitu kinacho endana na wewe ili uwe huru sehemu yoyote ile Na hapa ni kwa pande zote mbili kwa wadada na kaka zetu 

2 JUA  RANGI ZIPI ZINAKUPENDEZA ZAIDI

 Hapa kwenye rangi sasa ndugu zangu kuna watu mnajua kuvaa kachumbari bwana, rangi ya ngozi yako ndio itakupa jibu ni nguo za rangi gani uvae kama ni rangi za kung’aa au kupoa na unaweza kujua kwa kufanya research ndogo mtandaoni au kuwauliza wataalamu wa mitindo au hata make-up artist.

  1. KUWA NA VIATU VYA AINA MBALIMBALI

Kuna wengine wanapenda viatu vifupi au virefu basi kabati litajaa hivyohivyo tu hapana hauto kuwa stylish namna hio kwa maana kuna mavazi mengine yanahitaji viatu vya aina fulani tofauti na ulivyo navyo, sasa na ujue mahari pakuvalia hivyo viatu sio uvae viatu virefu sio mahari pake

  1. USIVAE ACCESSORIES NYINGI

Yaani siku hizi na hizo kacha basi tafrani yaani utakuta baadhi ya wakaka na wadada wanatwisha mizigo katika mikono yao mtu ana saa, mipete ya kila aina, kacha na bangili juu kheee jamana tafta kiti simple ambacho kitakufanya utokelezee my wangu.

  1. OMBA MSAADA KWA MTU WAKO WA KARIBU

Kama una rafiki au ndugu wa karibu ambae anajua maswala ya mitindo muombe msaada wa kwenda kununua nae mahitaji yako ya mavazi, ukiwa nae utapata ushauri kutoka kwake sio kama ukienda peke yako






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags