Mgombea wa chama tawala Bola Tinubu ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliokumbwa na utata mkubwa nchini Nigeria. Mwanasiasa huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 70 alipata 36% ya kura.
Huku Mpinzani wake mkuu Atiku Abubakar alipata 29%, na Peter Obi wa Labour 25%.
Tinubu ni mmoja wa wanasiasa tajiri Zaidi nchini Nigeria, na aliegemeza kampeni yake kwenye rekodi yake ya kujenga upya jiji kubwa zaidi la Lagos alipokuwa gavana.
Aidha Bola alishinda majimbo mengine mengi katika eneo alikozaliwa la kusini-magharibi, ambako anajulikana kama ''mbabe wa kisiasa". Huku kauli mbiu yake katika kampeni ikiwa "Ni zamu yangu".
Leave a Reply