Timberlake atumbuiza kwa mara ya kwanza baada ya kukamatwa

Timberlake atumbuiza kwa mara ya kwanza baada ya kukamatwa

Ikiwa zimepita siku chache tuu tangu mwanamuzika wa Marekani, Justin Timberlake kukamatwa na polisi akiwa amelewa, msanii huyo ametumbuiza kwa mara ya kwanza katika tamasha lake lilifonyika usiku wa kuamkia leo jijini Chicago nchini humo.

Wakati akiwa kwenye onesha lake la kwanza la ziara yake ya ulimwengu ya 'Forget Tomorrow' alifunguka na kueleza kuwa wiki hii ilikuwa ngumu kwa upande wake.

“Tumekuwa pamoja katika heka heka za kushoto na kulia, na imekuwa wiki ngumu kwangu, lakini mko hapa, kwa ajili yangu name nipo hapa kwa ajili yenu na niwahakikishie tuu hakuna kinachoweza kubadilika furaha yetu kwa sasa”

Justin Timberlake alikamatwa na polisi siku ya Jumanne Juni 18, 2024 baada ya kukutwa anaendesha gari akiwa amelewa katika bandari ya Sag, New York.

Hii si mara ya kwanza kwa Timberlake kukutwa amelewa kwani mwaka 2019 picha zake ziliwahi kusambazwa kupitia mitandao ya kijamii akiwa na mkewe Jessica Beil amelewa, ambapo siku chache baadaye mwanamuziki huyo alikili na kuomba radhi hadharani kufuatia na tabia yake ya ulevi kupindukia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags