Tiffany Haddish: niliwahi kuuza nguo zangu za ndani ili nipate maokoto

Tiffany Haddish: niliwahi kuuza nguo zangu za ndani ili nipate maokoto

Mwigizaji na mchekeshaji kutoka Marekani Tiffany Haddish amefichua kwamba wakati alipokuwa anajitafuta aliwahi kutangaza kuuza nguo zake za ndani katika mtandao wa kuuza bidhaa akidai kuwa nguo hizo ni za mwigizaji Halle Berry.

Haddish amefunguka hayo alipokuwa kwenye mahijiano yake na podcast ya ‘We Playin’ Spades’ akieleza kuwa alidanganya yeye ni mfanyakazi wa nyumbani kwa Berry hivyo anabidhaa za nguo za ndani za mwanadada huyo anaziuza.

“Hapo zamani nilipokuwa nikihangaika kupata pesa niliwahi kuuza nguo zangu za ndani kwenye Craigslist, nilijitambulisha kuwa naitwa Rosalinda nimfanyakazi wa nyumbani kwa Halle Berry nina bidhaa ya nguo za ndani za Berry chafu na ningepata dola 300 kama zingenunuliwa” amesema

Halle Berry ni mwigizaji mkongwe wa Marekani aliwahi kushiriki Miss World mwaka 1986 na alishika nafasi ya sita ameonekana katika filamu kama ‘Kidnap’, ‘Bruised’, ‘Kevin Hart: What Now?’, ‘The Union’ na nyinginezo.

Kwa upande wa Tiffany Haddish amewahi kuonekana katika filamu kama ‘Bad Boys: Ride or Die’, ‘Night School’, ‘Girls Trip’, ‘Haunted Mansion’ na nyinginezo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags