Thiago amalizana na Chelsea

Thiago amalizana na Chelsea

Beki na nahodha wa klabu ya #Chelsea, #ThiagoSilva ambaye pia alikuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Brazil amethibitisha kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.

Thiago akiwa na Chelsea amecheza mechi 151 akishinda mataji makubwa ya Uefa Champion League, Uefa Super Cup na Ubingwa wa dunia wa klabu ndani ya misimu minne.

Mchezaji huyo mwenye umri wa mika 39 aliingia klabuni hapo mwaka 2020 kutokea klabu ya #PSG amedai kuwa alitua Chelsea kwa lengo la kucheza msimu mmoja lakini amefikisha misimu hiyo minne

“Chelsea ina maana kubwa kwangu. Nilikuja hapa kwa nia ya kukaa mwaka mmoja tu na ikaishia miaka minne. Sio kwangu tu bali kwa familia yangu pia” amesema Thiago.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags