The Rock amnunulia nyumba mpiganaji wa UFC

The Rock amnunulia nyumba mpiganaji wa UFC

Muigizaji mashuhuri nchini Marekani Dwayne Johnson maarufu kama The Rock amemnunulia nyumba kama zawadi mpiganaji wa UFC, Themba Gorimbo jijini Miami baada ya kuguswa na stori yake ya kubakiwa na dola 7 tu kwenye akaunti yake ya benki.

Bondia huyo kutoka Zimbabwe hapo awali hakuwa na makazi na alikuwa akiishi na kulala kwenye kochi, katika eneo lao la kufanyia mazoezi.

Inasemekana kuwa, Themba alipiga mnada vifaa vyake vya kupigana alivyovitumia kwenye pambano lake alilopata ushindi, ili kufadhili uchimbaji kisima cha maji kijiji kwao nchini Zimbabwe






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags