Tetemeko la ardhi lamkuta ‘rapa’ Sean akiwa live

Tetemeko la ardhi lamkuta ‘rapa’ Sean akiwa live

‘Rapa’ kutoka #Jamaica #SeanPaul anadaiwa kusitisha mahojiano baada ya tetemeko la ardhi lililoikumba jengo la #Kingston nchini humo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vinaeleza kuwa ‘rapa’ huyo alikuwa akifanya mahojiano na msanii #TofuJack na producer wa muziki #DanZabludovsky, ndipo chumba kizima kikaanza kutetemeka ikapelekea kukatika kwa mawasiliano.

Hata hivyo inaelezwa kuwa msani huyo yupo salama na watu wengine, japo kumetokea uharibifu kidogo wa mali za watu katika kisiwa hicho.

Sean Paul anatamba na ngoma zake mbalimbali ikiwemo ya ‘Earthquake’ aliyo uachia mwaka jana.

.

.

#MwananchiScoop

#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags