Tetemeko la ardhi laingilia kati show ya Travis na Kanye

Tetemeko la ardhi laingilia kati show ya Travis na Kanye

Uwanja ambao limefanyika tamasha la ‘Rapa’ kutoka nchini Marekani Travis Scott ambalo alimualika mwanamitindo na muimbaji Kanye West, uwanja wa Kihistoria wa Circus Maximus, Italy unadaiwa kupatwa na tetemeko la ardhi.

Kwa mujibu wa shirika la habari la CNN linaeleza kuwa, Mkurugenzi wa uwanja huo alitoa wito wa kusitisha kwa matamasha karibu na eneo hilo, tamko hilo lilitolewa, baada ya Show ya Travis kuzua hofu kubwa ya Tetemeko la Ardhi eneo hilo.

Hofu ya tetemeko hilo imekuja baada ya Travis kumpandisha ‘stejini’ Kanye, na kupelekea mashabiki kupandwa na mizuka na kuanza kuruka ruka na kusababisha mtikisiko mkubwa, kwa mujibu wa kituo cha kupima tetemeko la ardhi (Seismic Station Italy), inadaiwa kuwa tetemeko hilo lina ukubwa wa 1.3 kutoka umbali wa kilometa 9, na eneo lililofanyika show.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags