Ten Hag na wachezaji wake wapigwa rungu

Ten Hag na wachezaji wake wapigwa rungu

Kocha wa klabu ya #ManchesterUnited, Erik ten Hag na wachezaji wake watalazimika kupunguzwa mishahara kama watashindwa kufuzu kwa Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Kwa mujibu wa The Sun News imeeleza kuwa klabu hiyo kwa sasa ipo nafasi ya 7 baada ya michezo 32 huku ikiwa na alama 16 nyuma ya klabu ya Aston Villa ambao wapo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Hiyo imekuja baada ya wachezaji na kocha wao kushuka viwango hivyo, timu hiyo ina haki zote za kuwakata mishahara yao kwa sababu mikataba yao ina vipengele vinavyowahitaji mshahara kupunguzwa kwa asilimia 25 endapo wakishindwa kumaliza katika nafasi nne za juu klabuni hapo.

Ingawa kwa sasa klabu hiyo ina mtazamia kwa ukaribu sana Ten Hag tayari wameweka wazi kuwa atapunguziwa kutoka pauni 9 milioni kwa mwaka hadi pauni 6.75 milioni.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags