Ten Hag ajitetea kisa majeruhi

Ten Hag ajitetea kisa majeruhi

Baada ya kufungwa na ‘klabu’ #NottinghamForest mabao 2-1, ‘kocha’ wa ‘klabu’ ya #ManchesterUnited, Erik Ten Hag, amejitetea kwa kusema kinachoimaliza ‘timu’ yake ni idadi kubwa ya wachezaji majeruhi iliyo nao.

Inaelezwa ‘mechi’ hiyo ilikosekana wachezaji kama Rasmus Hojlund, Luke Shaw, Casemiro, Victor Lindelof, Mason Mount, Harry Maguire na Lisandro Martinez ambao wote ni majeruhi.

Hata hivyo ‘kocha’ huyo anaamini ifikapo Januari mwakani ‘timu’ yake itakuwa bora kwani ‘mastaa’ hao watakuwa wamesharudi kwenye kikosi.

Man United kwa sasa inashika nafasi ya saba kwenye EPL, ikiwa imecheza ‘mechi’ 20, ikifunga 10, sare moja na kufungwa tisa.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags