Tems akosolewa kwa vazi la kuziba wenzake

Tems akosolewa kwa vazi la kuziba wenzake

Aloooooh! Sio powa wewe ukijiona umependeza wenzio wanakuona kituko basi bwana, Msanii kotoka nchini Nigeria Tems amekuwa gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya vazi lake ambalo lilizuia kuonekana kwa baadhi ya wahudhuriaji wengine kwenye usiku wa Tuzo za Oscar.

Mwanadada huyo aliteuliwa kwa wimbo bora wa Kiasilia kutoka katika movie ya  Black Panther: Wakanda Forever Lift Me Up.Gauni lake jeupe lililokuwa limezunguka kichwa chake lilishutumiwa baada ya picha ya skrini kuonyesha mgeni akikunja shingo yake ili kutazama jukwaani. kwawasiofahamu bwana vazi hilo au nguo ya mwimbaji huyo ilishonwa na mwanamitindo mzaliwa wa Ukraine, Lessja Verlingieri.

Ikumbukwe tuu msanii huyo alishinda Tuzo za Grammy mwezi Februari katika kitengo cha Best Melodic Rap Performance kwa mchango wake kwenye wimbo wa Wait for U akiwa na Future na Drake.
Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post