Taylor Swift apewa heshima na instagram

Taylor Swift apewa heshima na instagram

Ikiwa zimebaki siku chache tuu mwanamuziki kutoka nchini Marekani Taylor Swift kuachia album yake ya mpya iitwayo ‘The Tortured Poets Department’, msanii hiyo amepewa heshima na mtandao wa kijamii wa Instagram na Threads kwa kuwekewa feature ambayo haikuwahi kuwekwa kwa mtu yoyote yule.

Feature hiyo ambayo inaweza kukuonesha jina la album hiyo pamoja na muda uliyosalia kutolewa ambapo inayotarajiwa kutoka Aprili 19  ikiwa na nyimbo 16 huku ikitajwa kuwa na nyimbo tofauti ambazo ni The Manuscript, The Bolter, na The Albatross.

Kwa mujibu wa Billboard hii itakuwa album ya 11 kwa Taylor Swift hapo awali aliwahi kuachia album kama ‘Fearless (2008)’, ‘Taylor Swift (2006)’, ‘Speak Now (2010)’, ‘1989 (2014)’ na nyinginezo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags