Taylor aingia kwenye orodha ya mabilionea

Taylor aingia kwenye orodha ya mabilionea

Mwanamuziki kutoka nchini Marekani #TaylorSwift ameibuka kuwa miongoni mwa matajiri wakubwa duniani.

Kwa mujibu #Forbes imeripotiwa kuwa mwanamuziki huyo kwa sasa anamiliki utajiri binafsi wastani wa dola 1.1 bilioni ikiwa ni sawa Sh 2.5 trilioni huku idadi hiyo ya fedha ikimfanya kuwa mtu wa 2,545 kati ya 2,781 ya mabilionea wa mwaka 2024.

Hata hivyo anayeongoza orodha hiyo ni mfanyabiashara kutoka nchini Ufaransa Bernard Arnault ambaye anamiliki chapa ya LVMH akiwa anamiliki utajiri wa dola 233 bilioni.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post