TANZIA: Bernard Membe afariki dunia

TANZIA: Bernard Membe afariki dunia

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania, Bernard Membe (69) amefariki dunia leo Ijumaa, Mei 12, 2023 katika Hospitali ya Kairuki, Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi, Mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa hospitali hiyo, Arafa Juba amesema mwanasiasa huyo ambaye mwaka 2020 aliwania urais wa Tanzania kupitia ACT-Wazalendo amefikwa na mauti saa mbili asubuhi.

“Ni kweli Membe aliletwa asubuhi hapa akapatiwa matibabu na wataalam kama ilivyo kawaida mgonjwa anapokuja hospitali lakini Mungu alimpenda zaidi amefariki saa mbili asubuhi,” amesema Arafa.

Kuhusu ugonjwa uliokuwa unamsumbua, Arafa amesema ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari hivyo undani wa hilo unaweza kutolewa na familia na si hospitali.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags