Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) limefungia wimbo wa mwanamuziki Madee alioachia siku ya jana tarehe 13 Disemba, kutokana na wimbo huo kukiuka maadili.
Kwa mujibu wa barua iliyotolewa na Baraza hilo na kusainiwa na Katibu Mtendaji Dkt Kedmon Mapana imeeleza kuwa Madee alichapisha wimbo wenye maudhui yanayokiuka kanuni za BASATA za mwaka 2018 na mwongozo wa uzingatiaji maudhui katika kazi za Sanaa wa mwaka 2023.
Hivyo basi baada ya kujiridhisha Baraza hilo limemtaka msanii huyu kushusha wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali, kuufungia wimbo, kutopigwa au kuchezwa mahali popote, kutoucheza kwenye vyombo vya habari. Pia msanii huyo amepigwa faini ya tsh 3000,000 na kutofanya shughuli za Sanaa hadi atakapolipa faini hiyo.
Aidha katika barua hiyo imeonesha mzalishaji muziki Mr T Touchez naye ametozwa faini tsh 1000,000. Pamoja na muhusika aliyepandisha wimbo huo kwenye mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali atatakiwa kulipa faini 1000,000.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi
Leave a Reply