T-MARC Tanzania yasambaza Kondomu Milioni 60

T-MARC Tanzania yasambaza Kondomu Milioni 60

Shirika lisilo la kiserikali, T-MARC Tanzania limesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano iliyopita limefanikiwa kuuza na kusambaza kondomu Milioni 60 katika maeneo yote nchini.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Muwakilishi Mauzo wa shirika hilo, Oliveria Tarimo wakati wa kuhitimisha maonesho ya wiki moja ya siku ya Ukimwi duniani yaliyofanyika uwanja wa Ruandansovwe jijini Mbeya.

AlisemaT-MARC Tanzania lina jukumu ya kuhakikisha jamii inapata huduma za afya za kudumu na za uhakika kwa kushirikiana na washirika wake, hivyo wamekuwa wakifanya hivyo ikiwemo kuuza na kusambaza kondomu hasa kwa vijana abao wapo katika kundi hatarishi la kupata maambukizi ya VVU.

“Tumekuwa shirika ambalo tunafanya kazi kwa karibu na Serikali katika mapambano ya vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi na hiyo imedhihirishwa katika maonyesho ya wiki moja ya siku ya Ukimwi duniani huko Ruandansovwe, jijini Mbeya,” alisema

Alisema T-MARC Tanzania ilishiriki kwa kuwa na banda kwenye wiki ya maadhimisho hayo ambayo kwa mwaka huu yalikuwa na kauli mbiu inayosema “Zingatia Usawa. Tokomeza Ukimwi. Tokomeza Magonjwa ya Mlipuko”.

Tarimo alisema kutokana na kuwa mshirika wa karibu wa serikali ya Tanzania katika vita vya mapambano dhidi ya Ukimwi wameweza kufanya kazi zao kwa wwledi na kuifikia jamii husika.

Aidha alisema katika maonyesho hayo banda la T-MARC lilionekana kuwa kivutio kutokana na namna ambavyo walionyesha umahiri kwenye shughuli zake za huduma za afya ikiwemo mapambano dhidi ya Virusi vya Ukimwi, Kifua Kikuu, uzazi wa mpango, afya ya uzazi, lishe, Malaria, Maji, suala la usafi wa mazingira pamoja na kuhamasisha utoaji wa nafasi kwa mtoto wa kike katika maendeleo yake.

“Katika elimu waliyokuwa wakitoa T-MARC wameweza kueleza bayana kuhusu njia inayotumiwa zaidi kupata maambukizi ya Ukimwi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine ni ya kujamiana ambayo huchangia kwa asilimia 80,” alisema.

Alisema katika wiki hiyo ya maonesho T-MARC ilipeleka mafunzo ya kuhamasisha matumizi ya Kondomu zao pendwa za  Dume Classic, Dume Desire, na Dume Extreme, ambazo zinalenga rika mbalimbali na watu wenye kipato tofauti tofauti huku wakilenga vijana na watu walio kwenye sehemu hatarishi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags