Suge Knight adai Diddy ni FBI

Suge Knight adai Diddy ni FBI

Mwanzilishi mwenza wa rekodi lebo ya ‘Death Row Records’ kutoka Marekani Suge Knight, ambaye kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka 28 jela amedai kuwa mkali wa Hip-hop kutoka nchini humo Diddy Combs anafanya kazi na FBI kwa muda mrefu.

Ameyasema hayo kupitia podicast yake iitwayo ‘Collect Calls’ inayoruka moja kwa moja kutoka jela akidai kuwa Diddy amekuwa akitoa taarifa na kufanya kazi na vyombo vya sheria kama FBI kwa muda mrefu.

Knight alifunguka zaidi kwa kueleza kuwa Diddy ni mtoa taarifa wa milele na ndiyo maana linapokuja suala lake la kisheria mambo yanakuwa tofauti huku akidai kuwa wapo baadhi ya watu wanalifahamu hilo wakiwemo rafiki zake wa karibu pamoja na timu yake nzima.

Hii siyo mara ya kwanza kwa Diddy kuhusishwa kuwa mfanyakazi wa FBI kwani Mei 18 mwaka huu mtangazaji na mwanaharakati kutoka nchini Marekani, Candace Owens alidai kuwa msanii huyo hayupo jela mpaka sasa kwa sababu yeye ni FBI/CIA.

Diddy amekuwa akiandamwa na kesi saba mpaka kufikia sasa za unyanyasaji wa kingono tangu Desemba 2023 ambapo mpaka kufikia sasa wanasheria wake wanaendelea kupambana Mahakamani na kesi hizo.

Pia kufuatia na tuhuma hizi makazi ya Sean "Diddy" Combs, ya Los Angeles na Miami Machi 25, kufanyiwa upekuzi na Mawakala wa Usalama wa Taifa kama sehemu ya uchunguzi wa Serikali kuhusu madai ya biashara ya ngono yanayomhusisha msanii huyo.
.
.
.
#MwananchiScoop
#BurudikaNasi


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post