Straika aliyewafunga Yanga atajwa

Straika aliyewafunga Yanga atajwa

Kikosi cha Yanga kimerejea nchini jana ikitokea Ghana kucheza mchezo wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Medeama, lakini kuna mastaa wawili wameona kitu kwa mshambuliaji Jonathan Sowah na kushindwa kujizuia kwa kuutaka uongozi wa Yanga kufanya kila linalowezekana kumshusha nyota huyo.

Mastaa hao ni washambuliaji wawili wa zamani wa Yanga, Abeid Mziba ‘Tekero’ na Sekilojo Chambua waliowahi kufanya vizuri na timu hiyo ambao wote kwa pamoja wamepaza sauti wakimtaka Rais wa klabu hiyo Injinia Hersi Said kufanya kila linalowezekana kumsajili haraka mshambuliaji huyo ili kuwapunguzia stresi.

Sowah alicheza katika mechi hiyo ya Kundi D iliyopigwa mjini Kumasi na kufanikiwa kuifunga Yanga kwa mkwaju wa penalti, ikabla ya Pacome Zouzoua kulirejesha, lakini nyota huyo aliisumbua sana ngome ya vijana wa Miguel Gamondi iliyokuwa chini na nahodha Bakar Mwamnyeto, Ibrahim Bacca na Dickson Job.

Soma kwa undani kwenye tovuti ya Mwananchi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags