Steve Harvey akanusha kuwasema vibaya wachekeshaji

Steve Harvey akanusha kuwasema vibaya wachekeshaji

Siku chache zilizopita kupitia ukurasa wa X wa mchekeshaji na mtangazaji maarufu duniani Steve Harvey, kutoka nchini Marekani ulitumwa ujumbe ukiwa na taarifa yenye kudai kuwa wachekeshaji nchini humo hawachekeshi tena, jambo lililopelekea baadhi ya watumiaji wa mtandao huo kujitokeza na mitazamo tofauti.

Baadhi yao walianza kutaja majina ya wachekeshaji kutoka nchini humo ambao hawachekeshi tena, huku wengine wakidhani kuwa account ya Steve itakuwa imedukuliwa na aliyetuma ujumbe huo sio yeye kwani hawezi kuandika kitu kama hicho.

Sasa basi Steve ameamua kuondoa utata huo na kujibu mashabiki waliyoshitushwa na ujumbe huo kupia video aliyojirekodi, akidai kuwa yeye kazi yake kubwa ni kuwapa watu maneno ya kuwatia moyo na siyo kuwavunja moyo hivyo basi aliyeandika ujumbe huo si yeye bali ni mmoja wa wafanyakazi wake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post

Latest Tags