Spika wa bunge Marekani ajiuzulu

Spika wa bunge Marekani ajiuzulu

Kutoka huko nchini Marekani ambapo Nancy Pelosi, ambaye ameongoza chama cha Democrats katika Baraza la Wawakilishi la Marekani (Congress) kwa takriban miongo miwili, ametangaza kujiuzulu nafasi hiyo.

Pelosi mwenye umri wa miaka 82 ndiye mwanachama wa democrats mwenye nguvu zaidi katika Congress na mwanamke wa kwanza kuhudumu kama spika wa Bunge.

Ataendelea kuwakilisha jimbo lake ya California katika baraza la chini la Congress. Haya yanajiri huku Warepublican wakitarajiwa kutwaa tena udhibiti wa Bunge kufuatia uchaguzi wa katikati ya muhula.

Kevin McCarthy wa Republican ameshinda uteuzi wa chama hicho kuwa spika katika Bunge jipya la Congress na huenda akamrithi Bi Pelosi.

“Singewahi kufikiria kwamba siku moja ningetoka kwa mama wa nyumbani hadi kuwa spika wa Bunge,” Bi Pelosi alisema katika taarifa yake katika chumba hicho siku ya Alhamisi.

“Sitaomba kuchaguliwa tena kuwa uongozi wa Kidemokrasia katika Bunge lijalo. Saa imefika kwa kizazi kipya kuongoza chama cha Democrats,” alisema.

Bi Pelosi atahudumu kama spika hadi Januari wakati Bunge jipya litakapochukua mamlaka, na atasalia katika kiti alichochukua kwa mara ya kwanza mnamo 1987 hadi Januari 2025.


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post