Rafiki wa muda mrefu wa rapa na mfanyabiashara maarufu Marekani Jay-Z, Stephen A. Smith amemkingia kifua rapa huyo kwa kudai kuwa haamini tuhuma za ubakaji zanazomkabili.
Kupitia kipindi cha hivi karibuni cha ‘The Stephen A. Smith Show’ Smith amefunguka kuwa haamini tuhuma hizo kwani anamjua msanii huyo kwa zaidi ya miaka 25.
“Siwezi kuamini hata kwa sekunde moja kwamba angehusika na tuhuma kama hizi. Ubakaji? kwanza kabisa, siwezi kuamini hilo. Pili, msichana wa miaka 13? Hapana. Yeyote ambaye amewahi kuwa karibu na Jay-Z na kumjua, ameona jinsi anavyowatetea wale wasiojiweza kabisa kati yao ni watoto.
“Mtu ambaye nimemjua na kumpenda kwa zaidi ya miaka 25 siamini hata kwa sekunde moja angeweza kufanya jambo kama hilo. Hilo si kutojali, hiyo ni upendo wa kweli,”amesema Smith
Utakumbuka kuwa mapema wiki hii Jay-Z alituhumiwa kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 13 tukio ambalo linadaiwa kufanyika akiwa na Diddy mwaka 2000 baada ya sherehe za ugawaji wa tuzo za MTV.
Hata hivyo, masaa machache Jay-Z alikanusha tuhuma hizo huku akiweka wazi kusikitishwa na mwanasheria ambaye amefungua shtaka hilo bila kupepesa macho akiliita shtaka hilo ni upuuzi na lina lengo la kumkamua pesa na kumdhalilisha.
Leave a Reply