Slimsuma msanii anayeishi kwenye ndoto zake

Slimsuma msanii anayeishi kwenye ndoto zake

It’s another Friday ndani ya makala za michezo na burudani bwana, wiki hii tunachonga naye Ismail Nassir maarufu kama Slimsuma, kijana ambaye anajihusisha na muziki kizazi kipya.

Slimsuma ni kijana ambaye anaishi katika ndoto zake alizokuwa nazo tangu awali, akiwa anapigania zaidi hapo baadaye kuja kuwa msanii, mchezaji mpira au mwandishi wa habari.

Lakini amefanikiwa kutimiza ndoto zake hizo ambapo kwa sasa Slimsuma ni msanii wa muziki wa hip hop, licha ya kuwa ni mwanafunzi katika Chuo Tumaini University Campus ya Dar es salaam akichukua degree ya masomo ya Mass Communication, mwaka wa tatu.

Slimsuma amejikita zaidi katika uimbaji wa Muziki wa Hip Hop, ambapo nowadays vijana wengi chipukizi hususani walioko vyuoni wameonekana kuvutiwa zaidi na mtindo huu wa uimbaji.

Akizungumza na  Jarida la Mwananchi Scoop Slimsuma ameeleza sababu za vijana wengi kutumbukia kwenye mtindo huo wa muziki akidaikuwa namna unavyowasilishwa ujumbe wake ndiyo sababu kubwa ya watu kuukubali katika jamii.

Aidha alisema hip hop ni muziki ambao vijana wengi wanafanikiwa kupitia kazi ambazo wanazifanya, kwani mara nyingi maudhui na namna unavyowasilishwa huwa na mafunzo mbalimbali katika jamii.

Vile vile alizungumzia sababu za muziki huo kupendwa sana na jinsia ya kiume kuliko ya kike, akieleza kuwa wanawake wengi wanahofia kufanya muziki huo kulingana na kuimba au life style yake.

Hata hivyo amesema kuwa wananwake wanapaswa kujiamini kwani muziki huo sio kwa ajili ya wanaume bali ni  wa watu wote wadhubuti na watafanikiwa kwenye kazi zao.

Sambamba na hayo Slimsuma ameeleza ugumu anaoupata pindi anapoandika mistari katika nyimbo zake na kubainisha kuwa anapata ugumu wakati jinsi ya kupanga maneno na kuhakiksha lugha atakayoitumia ni nyepesi na jamii iweze kuifahamu kwa urahisi.

Aidha ameweka wazi kuwa sio kila msanii anaweza kuimba muziki huo, lakini pia sio kila anayefanya hi hop anaweza kuimba mtindo mwingine kwani inategemea na muimbaji mwenyewe jinsi alivyojikita zaidi

“Sio kila msanii anaweza kuimba hip hop na sio kila mwana hip hop anaweza kuimba mitindo mingine ya muziki ikiwemo singeli, RNB na mingine japo watu ambao wanaweza kufanya vyote lakini sio rahisi “alisema na kuongeza

“Wapo wana hip hop ambao wanaweza kuimba mitindo mingine na wapo wanaoimba mitindo mingine wanaweza kufanya hip hop pia hivyo always vicevesa is true na wapo watu ambao wanaweza kufanya vitu vyote kwa wakati mmoja “alisema.

Hata hivyo ameeleza changamoto kubwa ambayo inaikumba muziki huo akisema kuwa jamii imeweka dhana kuwa muziki huo ni wawanaume tu hivyo imesababisha hata wanawake hawaufuatilii sana muziki huo.

“Wanawake hawapo sana katika kuusuport muziki huu hivyo hata unavyoufanya unapata support kwa wanaume hivyo umetengwa na jinsia ya kike hivyo kunahitaji extral effort ili uweze kufika mbali zaidi”alisema

Sambamba na hayo Slimsuma hadi sasa amefanikiwa kutoa nyimbo takribani 9 ambapo hivi karibuni alitoa Ep yake yenye nyimbo 5ingawa awali alikuwa ameshatoa ngoma 4.

 Aidha ngoma mbayo ilibamba sana na kumtoa zaidi ni ile ya ‘Kumbe’ ambayo hakumshirikisha mtu yeyote.

Vile vile Slimsuma ni kijana mwenye malengo makubwa sana kupitia muziki wake ameeleza kuwa kiu yake kubwa ni kufanikiwa kwenye kitu anachokifanya.

“Muziki huu naufanya kwa malengo,  kitu chochote ambacho mtu unaenjoy kukifanya kuna ile hali ambayo unatamani uifikie, nataka muziki wangu ujikite zaidi kwenye kuelimisha jamii, kueleza matatizo yanayoikumba jamii na kuinsipire pia”alisema.

Umewahi kufikiria kuimba muziki wa mtindo mwingine? kama hapana kwanini ?! Na kama Ndiyo kwanini?!

“Yap nishafanya muziki kwa mtindo wa bongo fleva kwani mimi ni song writer pia lakini hapa ni suala la muda nafikiri muda ukifika nitazitambulisha kwa hadhira”anasema na kuongeza

“Ila kwa sasa nafanya hip hop kwani nataka nifahime zaidi kwa mtindo huo na niko free sana kuufanya tofauti na mtindo mwingine”alisema.

Hata hivyo Slimsuma ametoa ushauri wake kwa vijana ambao wanachipukia na wanaukubali sana muziki huo akiwataka kupamabna na kutokukata tamaa na waendelee kuufanya.

Aidha alisema licha ya ugumu ambao upo hawataikiwi kurudi nyuma hivyo wanatakiwa kusimamia malengo yao na kile ambacho wanakipigania ili waweze kufikia ndoto zao.

Historia ya Slimsuma kwenye muziki

Slimusuma alianza kujihusisha na masuala ya muziki baada ya kumaliza elimu yake ya kidato cha sita lita cha kuanza kuandika nyimbo tangu alipokuwa kidato cha kwanza.

“Niliamua kufanya hivyo kwani sikutaka kuchanganya shule na muziki kwasababu nilipokuwa form 3 nilijaribu kufanya muziki nikaona unahitaji mambo mengi sana hivyo nilistop kipindi hicho”anasema na kuongeza

“Nilianza kutoa nyimbo nilipofika chuo mwaka wa kwanza ndo nilianza kufanya harakati zote za muziki ila kuupenda muziki na kuufuatilia nilianza kitambo hata sikumbuki ni mwaka gani”alisema.  

 

 

 






Comments 2


  • Awesome Image
    Lydia

    Yo the guy yupo vizuri sana nimepitia nyimbo zake zote and i like each and every rhyme... ila ngoma ya KUMBE sio ya kitoto🔥🔥

  • Awesome Image
    Bigman iss

    Safi Sana suma

Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post